Let me talk to ya! Nataka kusema sana (No si sana) kuhusu watu wa aina
Fulani, mzeiya A.Y sema
Mikono juu, onyesha kama hufagilii mambo ya kishamba
Aah juu! Nyosha mikono ishara tumewapiga bao
I
Yatazame vyema macho yangu right now
Nishapitia mambo mengi hata zaidi yao
Unapong'ata kwangu na kupulizia kwao
Unapochoka zaidi baada ya kuona mi nacheka nao
(Oh) Leo nakupa ukweli baada ya kuona unanispy
Cheza nami mbali sitaki hata unisabahi
(Sikujui) Niaje nipoteze muda nikuchunguze
(Hunijui) Vipi utunge uzushi kwangu uyasambaze
Mind your business hujui style ya Maisha yangu
B**i sitaki ubishe hadi kwenye anga zangu
Kila siku unayafuatilia, nayoyahangaikia
Lakini huwezi kuniharibia
Usione nimeshhh ukataka kupima
Nilikuona mwema kumbe zzzz nishakusoma
Nikiwepo mtu poa, nikiondoka unanichoma
Sasa unapochoma kama unaoga nje mchana ah
Niko imara zaidi ya chuma cha pua
Sitabiriki ujio wangu moyo wako unajua
Mlango wa ngome yangu mjomba noma ngumu kuingia
Ndo maana bado mi nakamua border nyingi napasua
Bridge
Shida zangu kwani zinakuhusu nini (wewe)
Hata raha zangu zinakuhusu nini (wewe)
Pia Maisha yangu yanakuhusu nini (wewe)
OYAA X 2 (OYAA X 2)
Mikono juu, onyesha kama hufagilii mambo ya kishamba
Aah juu! Nyosha mikono ishara tumewapiga bao
II
Usione watu wamechill wametulia, Busy
B**i ukaona easy kuwachezea, ukidhi
Kupandikiza chuki news kudandia
Please, sitaki lawama kama vipi we potea
Fanya usepe tu kwangu, kwangu hupati kitu fool
Niogope kama OGOPA full wa mbuzi kama FID Q
(A.Y x2) Bado nafanya mema huh
Nikipata, nikikosa namshukuru Mungu tu
Kikulacho mbona kinguoni mwako
Wanaokuua mbona wa karibu yako
We unashangaa nani anauza file lako
Kama Adili kama mi (Bora niwe peke yangu)
Deal zako ka zinabuma b**i hasira usilete kwangu
Kama zali oh si lako jitume kibingwa wangu
Sio unakaa tu, kazi tu, kupiga majungu
Napo muda unapata bado unapiga virungu
Mchawi hana alama wapo (humuhumu)
Asiyependa uendelee ni (mchawi tu)
Hakosi uja kwako hodi kila saa (Ngo, ngo)
Ndani chuki nje kila saa anakupa tano. (Ngum, Ngum)
Bridge
Shida zangu kwani zinakuhusu nini (wewe)
Hata raha zangu zinakuhusu nini (wewe)
Pia Maisha yangu yanakuhusu nini (wewe)
OYAA X 2 (OYAA X 2)
Mikono juu, onyesha kama hufagilii mambo ya kishamba
Aah juu! Nyosha mikono ishara tumewapiga bao
(Aaah) Usijaribu kuchunguza sura hii
(Aaah) Kama ina raha ama zzzz
(Aaah) Usilete tabia za kizamani
Maisha yangu yanakuhusu nini
Au vipi bwana, Ni hayo
Huu ni muda na kila mtu kujiheshimu rafiki yangu
Haijalishi wewe ni nani na unatoka wapi
Niachie mimi nifanye kama mimi
Sababu siwezi kufanya kama wewe na wewe huwezi kufanya kama mimi
Sikiliza Ambwene, hili ni bonge la dude, bonge la beat kutoka kwa OGOPA
Matrack kama haya yanatakiwa kusikilizwa mtaani. Chuki kibao zipo, kwa nini?
USICHUKULIE POA X 2