menu-iconlogo
huatong
huatong
mbosso-amepotea-cover-image

Amepotea

Mbossohuatong
rockrashihuatong
เนื้อเพลง
บันทึก
Vipeperushi vinasambaa

Eti natafutwa

Nimepotea wiki imekataa

Ndugu wamechachamaa

Wananitafuta

Nimepotea mwezi umekata

Kazini sionekani, yupo wapi huyu

Simuni sipatikani, yupo wapi huyu

Baba kaniulizia, yupo wapi huyu

Mama aishi kulia, yupo wapi huyu mimi

Nimezama katika kina kirefu

Cha bahari ya mapenzi

Nimezama katika kina kirefu

Cha bahari ya mapenzi

Sio ya Andit Purre mwana Rajab mlomkuta Tanga

Sijafanywa msukule msipate tabu kumaliza waganga

Amenirudisha shule hesabu maumbo kupanga

Penzi la wasasambule lenye protini, vitamin na wanga

Aaaah! ladha yake, si sukari

Ni vichenza na malimao

Mechi zake, huwa hatari

Ni chenga na mabao

Kazini sionekani, yupo wapi huyu

Simuni sipatikani, yupo wapi huyu

Baba kaniulizia, yupo wapi huyu

Mama aishi kulia, yupo wapi huyu mimi

Nimezama katika kina kirefu

Cha bahari ya mapenzi

Msinitafute, nimezama (Msihangaike katika kina kirefu)

Nipo salama, (Cha bahari ya mapenzi) salama, salama mimi

Nipo salama mimi, Nipo salama mimi

Msinitafute, Nipo salama mimi

เพิ่มเติมจาก Mbosso

ดูทั้งหมดlogo