menu-iconlogo
logo

Mapenzi

logo
Lời Bài Hát
No aah, aah

(Mr. Saimon)

Aya aah aah eeh eh eh

Amini unaempenda, naye ana wake anayaempenda pia

Na siku zinakwenda aah aah

Na hata yule anayempenda, naye ana wake anayemwita dear

Haya mapenzi mwana kwenda aah

Na ni yaleyale mapenzi

Yalotesa mabibi na mababu hadi leo

Mie mwenzenu siyawezi

Ni bora uyashuhudie kwa mwenzio, ama kwa video

Usione mtu analiaga, ukadhani ni utoto

Mapenzi yana vingi vituko, nyingi changamoto ona

Ukimpata anayekuthamini

Mnatulia na utunze yake heshima

Ujue ndo kashazama kwa kina wewe

Ah eeh vipo vya kuvumilia

Lakini sio mapenzi, mapenzi yanaumiza

Mi ndio maana siyawezi

Vipo vya kuvumilia

Lakini sio mapenzi, mapenzi yanaumiza

Mi ndio maana siyawezi

Aah we penda unapopenda, unapoamini

Kwamba amani ya moyo wako ipo

Na ukikosa unachopenda, utapagawa bure

Hata ufanye matambiko

Hata ukipenda kweli, hauwezi jua sababu ni siri ya moyo wako

Hata kama akifeli, atapuuzia ili uteseke tu peke yako

Ngoswe kitovu cha uzembe, ukipenda huoni

Na anayempenda hajui, hatambui kama ye ndo ako mbooni

Hata akisema amechoka, anataka muachane

We zidi kumpenda tu hivyo hivyo

Maana mapenzi hayana mwenyewe aah

Unaweza ukaondoka, ukaenda kupenda pengine

Napo ukakuta ndivyo sivyo, ukajihisi una mkosi wewe aah

Ukimpata anayekuthamini mnatulia na utunze yake heshima

Ujue ndo ukashazama kwa kina wewe

Ah eh vipo vya kuvumilia, lakini sio mapenzi

Mapenzi yanaumiza, mi ndio maana siyawezi

Vipo vya kuvumilia, lakini sio mapenzi aah eh

Mapenzi yanaumiza aah, (mi ndio maana siyawezi)

Ibraah, Konde Music Worldwide

This is Saimon, uuh

Mapenzi của Ibraah - Lời bài hát & Các bản Cover