menu-iconlogo
logo

Yatapita

logo
Letras
Yatapita yana mwisho

Ipo siku tutayasahau

Watatuheshimu walio tudharau

Kaza moyo, nivumilie

Amini tutayasahau

Watatuheshimu walio tudharau wote

Na ntakununulia vyote

Mawigi na simu vyote

Ntakuzawadia vyote

Pochi zenye thamani vyote

Nawe uende waringishia vyote

Utembee kwa uskani vyote

Na vioo ukiwafungia vyote

Aloiumba leo ni mungu na ndio ataiumba kesho

Amini fungu letu laja haliko mbali

Alisema mtazaa kwa uchungu, tutatafuta kwa mateso

Baby mitihani kawaida usijali, mnh

Kidogo nnachokuletea usinune pokea

Nipate moyo nifariji

Na juhudi naziongezea usichoke niombea

Molah atubariki zaidi

Mungu kakupa sura kakupa shepu

Nyuma chura mambo yetu

Mwana wa sanura, mwenzako mimi I love you

Umeniteka medula niko fyetu

Akili haina ndala Iko peku

Umenivurura, mwenzako mimi I love you

Ooh nivumilie

Yatapita yana mwisho

Ipo siku tutayasahau

Watatuheshimu walio tudharau

Kaza moyo, nivumilie

Amini tutayasahau

Watatuheshimu walio tudharau wote

Na ntakununulia vyote

Mikufu na simu vyote

Ntakuzawadia vyote

Pochi zenye thamani vyote

Nawe uende waringishia vyote

Utembee kwa uskani vyote

Na vioo ukiwafungia vyote

Ooh baby

Tazama nyota na mbalamwezi zatutazama

Liliwaka jua zikafanya subira mnh

Nhh

Na nnapokosa niambie mupenzi sio kuzozana

Nyumba haijengwi kwa vita hasira

Kwenye macho yako nikiyatazama

Naiona huruma yako mama

Changamoto maana kuna muda unakata tamaa

Nanoa kisu hatuli nyama

Na kodi lundo zatuandama

Riziki zama kwa zama

Ya kwetu kesho ya kwao ni jana

Kidogo nnachokuletea usinune pokea

Nipate moyo nifariji mnh

Na juhudi naziongezea usichoke niombea

Molah atubariki zaidi

Yatapita kipenzi changu

Yatapita yana mwisho

Ipo siku tutayasahau

Watatuheshimu walio tudharau

Kaza moyo, nivumilie

Amini tutayasahau

Watatuheshimu walio tudharau wote

Na ntakununulia vyote

Mawigi na simu vyote

Ntakuzawadia vyote

Pochi zenye thamani vyote

Na wewe uende waringishia vyote

Utembee kwa uskani vyote

Na vioo ukiwafungia vyote

Mungu kakupa sura kakupa shepu

Nyuma chura mambo yetu

Mwana wa sanura

Mwenzako mimi I love you